Kipare (Papua)

Kipare ni lugha ya Kivuka-Guinea Mpya nchini Papua Guinea Mpya inayozungumzwa na Wapare. Isichanganywe na lugha ya Kipare izungumzwayo nchini Tanzania. Mwaka wa 1990 idadi ya wasemaji wa Kipare imehesabiwa kuwa watu 2000. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kipare iko katika kundi la Kiawin-Pare.


From Wikipedia, the free encyclopedia ยท View on Wikipedia

Developed by Tubidy